Maadhimisho ya siku ya kutokomeza fistula nchini Uganda
Wakati dunia imeadhimisha siku ya kutokomeza fistula duniani Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu UNFPA, katika ripoti yake limesema kwamba takriban wanawake milioni 2 katika bara la Afrika, bara Asia na ukanda wa Uarabuni na Amerika ya kusini na Caribea wanaishi na majeraha na kuna visa kati ya 50,000 hadi laki moja kila mwaka, licha ya kwamba fistula inaweza kuzuiliwa. UNFPA imesema uwepo wa ugonjwa huo ni ishara ya doa katika mifumo ya afya katika kukabiliana na mahitaji ya wanawake. Kampeni ya kutokomeza fistula iliyozinduliwa na UNFPA na wadau mwaka 2003 sasa iko katika mataifa ya bara Afrika na kwingineko ambako Uganda ni moja ya nchi zilizoadhimisha siku hii. Basi ungana na John Kibego kutupatia yaliyojiri katika maadhimisho hayo nchini Uganda.