Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna Mkuu Zeid ataka ujumbe mkali kwa Burundi

Kamishna Mkuu Zeid ataka ujumbe mkali kwa Burundi

Bado jamii ya kimataifa inaweza kuzuia Burundi isielekee tena kwenye janga la zamani, amesema leo Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Zeid Ra’ad Al Hussein, akizungumza wakati wa mkutano wa maandalizi ya kikao cha 29 cha Baraza la Haki ya Binadamu kitakachoanza tarehe 15 mwezi Juni mwaka huu mjini Geneva, Uswisi.

Bwana Zeid amekaribisha jitihada za Muungano Afrika, mkutano wa kimataifa wa maziwa makuu, Jumuiya wa Afrika Mashariki, Muungano wa Ulaya na Umoja wa Mataifa katika kutatua mzozo huo kwa kuheshimu haki za binadamu, akisema anatumai baraza hilo litatoa ujumbe mkali ili kusitisha ghasia kwa kuwa...

Wakati wa ziara yangu nchini Burundi mwezi uliopita, nimeshtushwa na ukatili wa wanamgambo wa Imbonerakure, ambao wanaunga mkono serikali ya Rais Nkurunziza. Wanasiasa wa upinzani, waandishi wa habari, wanaharakati wa haki za binadamu na kwa kusema kweli raia wengi wa kawaida bado wanahofia maisha yao.”

Halikadhalika, katika hotuba yake, Kamishna Mkuu ameipongeza Tunisia kwa kufanikiwa katika wakati wa mpito na kuridhia sheria mpya kuhusu haki za binadamu.

Aidha amezungumzia tatizo la uhamiaji barani Ulaya na Asia Kusini, akisema lazima kipaumbele kiwekwe katika kutunza haki za wahamiaji hao kwa kuwaokoa baharini, kuwapatia hifadhi na kupambana na ubaguzi.

Hatimaye Kamishna Zeid ameeleza wasiwasi wake juu ya hali ya raia wanaokumbwa na ukiukaji wa haki za binadamu nchini Sudan Kusini, huku mapigano yakiendelea.