Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yasitishwe wakulima wavune Syria: WFP

Mapigano yasitishwe wakulima wavune Syria: WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limetaka kusitishwa kwa mapigano nchini Syria ili kutoa mwanya kwa wakulima kuvuna na kusafirisha mazao ili kuwafikia raia nchini humo walioko katika uhitaji wa chakula.

Akihutubia bodi ya WFP mjini Roma Italia, Mkurugenzi Mkuu wa WFP Ertharin Cousin amesema kuna viashiria kuwa mavuno ya mwaka huu wa 2015 nchini Syria yaweza kuwa mengi ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita wakati huu ambapo nchi iko katika hali ya sintofahamu ya usalama huku raia wakipoteza makazi.

Ameongeza kuwa ni muhimu mazao hayo yasipotee na chakula kipatikane kwa mahitaji ya nchi nzima