Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akiwa Ireland apongeza hatua za kusaidia wahamiaji:

Ban akiwa Ireland apongeza hatua za kusaidia wahamiaji:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyeko ziarani barani Ulaya amezunguzma na waandishi wa habari huko Dublin, Ireland na kupongeza nchi hiyo kwa harakati zake za kuwapatia makazi wahamiaji kutoka Mashariki ya Kati na Afrika.

Amesema hayo alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu suala la wahamiaji Afrika Kaskazini ambapo amesema wakati wa ziara yake nchini Ireland amepata fursa ya kukutana na watu kati ya 30 na 40 ambao wamehamia nchini humo kwa usaidizi wa serikali na wananchi.

Ban amesema wahamiaji hao wanatoka Syria, Afghanistan, Myanmar na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na kwingineko ambapo katika nyuso zao ameona wana matumaini na mustakhbali wao huku wakiwa na hofu na hali ya jamaa na familia zao kule walikotoka.

(Sauti ya Ban)

“Nashukuru kwa dhati na napongeza uongozi wa upendo na wema na kutjitoa wa serikali ya Ireland ya kuwapatia makazi wahamiaji nchini humu.nafahamu kuwa mna mpango mwingine wa kuwapatia makazi nchini humu watu wengine zaidi wapatao 300.”

Hata hivyo Katibu Mkuu amesifu hatua za Muungano wa Ulaya kwa usaidizi kwa wahamiaji huku akisema Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa wataendelea kushughulikia visababishi vinavyofanya watu kuhatarisha maisha yao baharini ili kusaka usalama ugenini akigusia bahari ya mediteranea na ile ya Andaman.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Ireland Enda Kenny.