Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini Tanzania, watoto wazungumzia usalama wao barabarani

Nchini Tanzania, watoto wazungumzia usalama wao barabarani

Jarida hili maalum linaangazia usalama wa watoto barabarani, wiki ya usalama barabarani ikiadhimishwa duniani kote mwezi huu wa Mei, kauli mbiu yake ikiwa: okoa maisha ya watoto!

Katika ujumbe wake kwa wiki hiyo, Shirika la Afya duniani WHO limesema watoto wanazidi kuwa wahanga wa ajali za barabarani.

Utafiti uliofanywa na WHO umeonyesha kuwa asilimia 95 ya vifo vya watoto barabarani vinatokea kwenye nchi zinazoendelea au zenye kipato cha kati kwani watoto wanaenda shuleni kwa mguu na barabarani wanakopita hakuna miundombinu ya usalama ikiwemo vivuko vya pundamilia.

WHO pia kwenye maadhimisho hayo imewasilisha azimio la watoto kuhusu Usalama Barabarani likiwasihi viongozi duniani kuchukua hatua ili kunusuru maisha yao na kuhakikisha usalama wa barabarani.

Je nchini Tanzania hali ikoje? Tuungane na Gertrude Clement, mtoto mwanahabari wa miaka 15 kutoka mtandao wa watoto wanahabari Mwanza, mtandao unaoratibiwa na shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia watoto, UNICEF.