Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake na watoto watumiwa zaidi katika mashambulizi Nigeria :UNICEF

Wanawake na watoto watumiwa zaidi katika mashambulizi Nigeria :UNICEF

Idadi ya wanawake na watoto wanotumiwa kama silaha za  mauaji ikiwamo mabomu imeongezeka kaskazini mwa Nigeria mwaka huu ikilinganishw na mwaka jana kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Genevava Mwakilishi wa UNICEF nchini Nigeria Jean Gough amesema mwaka jana mashambulizi 26 yaliyohusishwa na wanawake na watoto  yaliripotiwa ambapo mwaka huu ikiwa ni mwezi May tayari matukio 27 yameripotiwa.

Amefafanua madhara yanayokabilikundi hilo kwa kutumiwa kama silaha za mashambulizi

(SAUTI JEAN)

“Watoto wengi wametenganishwa na familia zao wanapokimbia mashambulizi wakiwa hawana mtu anayewaangalia. Bila ulinzi wa famiali zao watoto hawa wako katika hatari kubwa ya kunynyaswa na watu wazima na hili laweza kuwasababishaia kufanya uhalifu au kufanya kazi na   vikundi vyenye silaha.

UNICEF nchini Nigeria kwa kushirikiana na mamlaka za kitaifa inaainisha watoto wasio na wazqzi au ndugu na kuwaopatia huduma  ambapo hadi sasa zaidi ya watoto 35,000 wameshapatiw amsaada wa kisaikolojia baada ya kuathiriwa na machafuko.