Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki unaleta mabadiliko katika jamii

Muziki unaleta mabadiliko katika jamii

Muziki ni sanaa ambayo kwayo iwapo itatumiwa vizuri italeta mabadiliko siyo tu kwa jamii ambayo inasikiliza bali pia kwa watunzi na waimbaji wenyewe. Hata hivyo kwa nchi zinazoendelea ikiwemo zile za Afrika Mashariki bado manufaa kutokana na muziki  yanasalia changamoto kutokana na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa wasanii kuhusu haki zao hususan hakimiliki jambo ambalo sasa shirika la Umoja wa Mataifa la hakimiliki, WIPO linapigia chepuo. Hii ni kwa kuwa ukosefu wa mbinu endelevu za kunufaika na muziki zinakwamisha wasanii husika kama inavyosimulia makala hii ya Assumpta Massoi akijikita zaidi kwa Suzana Owiyo, mwanamuziki kutoka Kenya.