Lazima kutokomeza fistula katika kipindi cha kizazi kimoja: Ban

Lazima kutokomeza fistula katika kipindi cha kizazi kimoja: Ban

Kesho tarehe 23, Mei, ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza fistula, Katibu Mkuu wa Umoja  wa Mataifa Ban Ki-moon amewasihi viongozi wa dunia kujituma zaidi ili kutokomeza janga hili. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.(Taarifa ya Priscilla)

Katika taarifa yake, Bwana Ban amesema kila nchi inayokumbwa na tatizo hilo inapaswa kuunda mkakati jumuishi wa kitaifa, ambao utalenga kutokomeza fistula katika kipindi cha kizazi kimoja. Aidha ameiomba jamii ya kimataifa kuongeza misaada yake kwa nchi zenye mahitaji zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu UNFPA, Babatunde Osotimehin, amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana, mathalan kwa wanawake 47,000 waliofanyiwa upasuaji wa kuponesha fistula, bado juhudi zinahitajika ili kupeleka huduma za afya za uzazi katika jamii duniani kote, kwani bado visa 50,000 hadi 100,000 vya fistula vinatokea kila mwaka.

Clement Ndahani ni meneja wa mpango wa Fistula wa taasisi ya afya ya CCBRT inayofanya kazi kwa kuwezeshwa na UNFPA nchini Tanzania