Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzingatie zaidi wajibu wa serikali kuhakikisha usawa na ubora wa elimu- mtaalam wa UM

Tuzingatie zaidi wajibu wa serikali kuhakikisha usawa na ubora wa elimu- mtaalam wa UM

Wajibu wa serikali wa kuhakikisha elimu bora na jumuishi unapaswa kuwa nguzo ya ajenda ya elimu baada ya mwaka 2015, amesema Mtaalam Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kupata elimu, Kishore Singh.

Bwana Singh amesema hayo mwishoni mwa kongamano la dunia kuhusu elimu la 2015, ambalo liliwaleta pamoja zaidi ya viongozi 130, likilenga kuweka barabara ya elimu ya dunia hadi mwaka 2030.

Mtaalam huyo amesema kuwa kwa kuzingatia kanuni za haki ya jamii, mikakati ya elimu ni lazima ikabiliane na ukosefu wa usawa, kwa kutilia maanani wasichana na wanawake, makundi ya kabila za walio wachache, watu wenye ulemavu, watoto wanaoishi katika maeneo ya migogoro, vijijini na katika mitaa duni mijini.

Amesema mikakati hiyo inapaswa pia kujikita zaidi katika kuendeleza usawa wa jinsia.