Ulimwengu usipobadili jinsi unavyokabiliana na dharura, kuna hatari ya Ebola tena- WHO

Ulimwengu usipobadili jinsi unavyokabiliana na dharura, kuna hatari ya Ebola tena- WHO

Jamii ya kimataifa inapaswa kubadili haraka jinsi inavyokabiliana na dharura za kiafya iwapo inataka kuepukana na janga jingine kama Ebola, wameonye wataalam wa Shirika la Afya Duniani, WHO.

Ikitoa onyo hiyo, WHO imesema kuwa mlipuko wa Ebola haujamalizika Afrika ya Magharibi..

Mlipuko wa homa ya Ebola umewaua zaidi ya watu 11,100, hususan katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

WHO imesema mifumo hafifu ya ya afya katika nchi hizo inahitaji uwekezaji mkubwa kutoka nje.

Dr Ruediger Krech kutoka WHO amesema, jamii ya kimataifa ilikimbilia kuuzima moto wa Ebola, lakini imeshindwa kufikiria jinsi ya kuuzuia usiibuke tena.

Tunasubiri moto uwake, tunakimbia kuuzima, lakini tunasahau kuweka kinga dhidi yake. Tunapaswa kubadili hilo, na tunatoa wito kwa jamii ya kimataifa iunge mkono juhudi za kujikita kwa mfumo wa huduma za afya kwa ujumla badala ya kumulika tu magonjwa makubwa, ili janga jingine kama la Ebola lisitokee tena kamwe.”

Katika mkutano na waandishi wa habari, afisa huyo wa WHO amesema ni muhimu kujenga mifumo ya afya Guinea, Liberia na Sierra Leone ambayo ni dhaifu, ili kuhakikisha