Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tofauti za utamaduni kwa maendeleo: #Unite4heritage

Tofauti za utamaduni kwa maendeleo: #Unite4heritage

Wakati leo ni siku ya kimataifa ya kutambua tofauti za utamaduni kwa ajli ya mashauriano na maendeleo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limesema ni fursa nzuri ya kutumia tofauti hizo za kitamaduni na lugha kujiimarisha badala ya kudhoofishana.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova katika ujumbe wake amesema kila uchao jamii inashuhudia uhalifu dhidi ya turadhi na mali za kitamaduni ambazo badala ya kushambuliwa zinapaswa kuenziwa kwani ni ishara ya utajiri wa eneo husika ambao unaweza kuwa kivutio kwa wengine na kuinua uchumi wa jamii.

Nchini Kenya, katika kuadhimisha siku hii kumefanyika mjadala maalum kuhusu utamaduni na maendeleo kwa ajili ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015 ambapo Dkt. Mzalendo Kibunjia, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Kenya anasema ni wakati muafaka kwa kuwa..

(Sauti Dkt. Kibunjia)