Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yarejesha msaada wa chakula Libya

WFP yarejesha msaada wa chakula Libya

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limerejesha usaidizi wa chakula kwa watu waliopoteza makazi yao kutokana na mzozo unaoendelea nchini Libya.Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Mratibu wa misaada ya dharura wa WFP nchin Libya Wagdi Othman amesema watu hao wamekuwa muda mrefu bila vyakula muhimu na mpango wa sasa ni kusambaza misaada hiyo muhimu kwa wakimbizi wa ndani 243,000 ndani ya miezi sita ijayo.

Bwana Othman amesema usambazaji huo ufanyika kwa ushiriiano na mdau wao nchini humo, STACO, ambapo wanasambaza vyakula kama vile tambi, mchele kwenye miji ya Wadi ash-Shati, Misrata, Sebha na Traghen.

Kwa sasa WFP imekuwa inatoa msaada huo kwa wakimbizi wa ndani 51,000 magharibi mwa nchi hiyo ambao walikuwa hatarini zaidi.