Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanamuziki Akon ashiriki mkutano kuhusu nishati New York

Mwanamuziki Akon ashiriki mkutano kuhusu nishati New York

Mpango wa jitihada ya upatikanaji wa nishati ya umeme kwa wote umezinduliwa leo mjini New York ambapo wadau wa nishati akiwamo mwanamuziki mashuhuri Akon Thiam wamewaleza waandishi wa habari juhudi za kuhakikisha nishati hiyo inawafikia watu hususani katika nchi zinazoendelea.

Wadau hao wamesema uwezeshaji wa kifedha kwa miradi katika nchi 20 zinazoendela ni moja ya mikakati ya kufikisha nishati umeme kwa kila mtu lakini wakasema juhudi zaidi zinahitajika.

Akiongea katika mkutano huo msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu nishati endelevu Dk. Kandeh Yumkella amesema ni furaha kuona kuwa upatikanaji wa nishati endelevu umeingizwa katika ajenda ya maendeleo kwa mwaka 2015 ikiwa ni lengo namba saba na kuongeza..

(SAUTI DK KANDEH)

"Ni hakika kuwa huwezi kuwa na hospitali bila nishati, huwezi kusukuma maendeleo ya kiuchumi bila nishati, watoto hawawezi kusoma usiku bila nuru."