Baraza la Afya Duniani laafikia mkakati wa kupambana na malaria

Baraza la Afya Duniani laafikia mkakati wa kupambana na malaria

Nchi wanachama wa WHO leo zimeafikia mkakati mpya wa kimataifa wa kupambana na malaria kuanzia 2016 hadi 2030, pamoja na kupitisha bajeti ya shughuli za 2016-2017.

Mkakati huo unalenga kupunguza mzigo wa ugonjwa wa malaria duniani kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020, na kwa asilimia 90 kufikia mwaka wa 2030.

Aidha, mkakati huo unalenga kutokomeza malaria katika nchi mpya zipatazo 35 ifikapo mwaka 2030. Kati ya mwaka 2000 na 2013, kiwango cha vifo vitokanavyo na malaria duniani kilianguka kwa asilimia 47.

Kwa mujibu wa WHO, mamilioni ya watu bado hawana uwezo wa kuzuia au kutibu malaria, na vifo vingi vinatokea bila kuripotiwa au kurekodiwa. Mnamo mwaka 2013, watu wapatao 584,000 walifariki kutokana na malaria.