MINUSMA yalaani shambulizi dhidi ya makazi ya wafanyakazi wake Bamako

20 Mei 2015

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA umelaani vikali shambulio la usiku wa kuamkia leo kwenye makazi ya watendaji wake yaliyoko mji mkuu Bamako.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani, naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema katika tukio hilo mtu asiyefahamika alimpiga risasi na kumjeruhi mlinzi mmoja raia wa Mali aliyekuwa anazuia jaribio la kutia moto gari la MINUSMA lililokuwa limeegeshwa nje ya makazi hayo.

Amesema mabomu mawili yalibainika baadaye kwenye eneo hilo na kwamba..

(Sauti ya Farhan)

Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa  unasisitiza kuwa mashambulio yoyote dhidi ya wafanyakazi wake na maeneo yake ni uhalifu wa kiwango cha juu na ni wajibu wa mamlaka za Mali kuhakikisha usalama wa wafanyakazi hao. MINUSMA pia inatiwa wasiwasi na ongezeko la ghasia kwenye maeneo mengi kaskazini mwa nchi hiyo na inasihi pande zote husika kurejesha utulivu na kusongesha mbele mchakato wa amani.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud