Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku tano za usitishaji mapigano hazitoshi kuwasaidia Wayemen wote:WFP

Siku tano za usitishaji mapigano hazitoshi kuwasaidia Wayemen wote:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeonya kuwa usitishaji wa karibuni wa mapigano kwa siku 5 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu Yemen haukutosha kuwafikia watu wote wanaohitaji msaada wa chakula na mahitaji mengine , na linaomba kuwepo kwa utaratibu unaoelewa wa vipindi vya usitishaji mapigano ili kuwapelekea msaada watu wanaouhitaji haraka.

WFP imegawa chakula kwa watu zaidi ya 400,000 katika muda was aa 72 za usitishaji mapigano na imefanikiwa kufika katika maeneo ambayo awali yalikuwa hayafikiki, lakini idadi hiyo ni nusu tuu ya watu 738,000 iliyotumai kuwafikia.

Mwakilishi wa WFP nchini Yemen Purnima Kashyap amesema katika kipindi hicho kifupi walihaha kufikia maeneo yaliyokuwa na mapigano na waliweza kufikia nusu tu ya maeneo waliyotaka kutkana na  wasafirishaji wa misaada kusita kupeleka malori yao katika maeneo ambayo mapigano na uvurumishaji wa makombora ulikuwa unaendelea.

WFP imesema inataka sitisho la mapigano la kueleweka kwenye maeneo yenye mapigano ili kuwezesha wadau wake kufikisha misaada ya chakula kwa watu wengi zaidi.