Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sakata Burundi, mwanamke ajifungulia kwenye boti, majaliwa yake sasa ni usaidizi

Sakata Burundi, mwanamke ajifungulia kwenye boti, majaliwa yake sasa ni usaidizi

Athari ya sintofahamu ya kisiasa inayoendelea nchini Burundi kufuatia bunge la nchi hiyo kumtangaza Rais Pierre Nkurunzinza kuwania nafasi ya Urais kwa awamu ya tatu, imeendelea kuongezeka na hata kugusa vizazi tarajiwa nchini humo. Mathalani wanawake wajawazito wamejikuta katika mazingira hatarishi siyo tu kwao bali pia watoto wao wanaojifungua na hata kuweka njia panda matarajio ya familia kuongeza uzao duniani.

Je kulikoni? Ungana na Sawiche Wamunze, afisa mawasiliano wa shirika la mpango wa idadi ya watu nchini Tanzania katika mahojiano yake na mume wa mwanamke mmoja aliyejifungua akiwa safarini kuvuka Ziwa Tanganyika kuingia Tanzania.