Wapagazi 20,000 wafikisha misaada kwa jamii zilizojitenga Nepal: WFP

Wapagazi 20,000 wafikisha misaada kwa jamii zilizojitenga Nepal: WFP

Shughuli za kuokoa maisha ya watu katika jamii zilizoko milimani nchini Nepal zinaendelea ikiwa ni wiki tatu baada ya tetemeko la ardhi lililoitikisa nchi hiyo.

Shughuli hizo zinahusisha wapagazi 20,000 kama sehemu ya operesheni ijulikanayo kama mountain express, na kila mpagazi anatarajiwa kubeba mgongoni kilo 30 za msaada kuwafikishia watu kwenye maeneo yasiyo na fursa ya barabara, limesema shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

WFP imeongeza kuwa lengo ni kuwafikia watu 45,000 kuanzia katikati ya mwezi Juni hadi Septemba lakini mashirika ya Umoja wa Mataifa ynasema ombi lake la dola milioni 150 kwa ajili ya Nepal limefadhiliwa asilimia 7 tu. Elisabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA BYRS)

“Ni operesheni nzito inayofanyika katika vijiji vilivyo ndani zaidi kwa ushirikiano na chama cha watembea kwa miguu Nepal na chama cha wapanda milima nchini Nepal.”

Lengo ni kuwafikia watu 45,000 kuanzia katikati ya mwezi Juni hadi Septemba lakini mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema ombi lake la dola milioni 150 kwa ajili ya Nepal limefadhiliwa asilimia 7 tu.