Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA, wadau wahaha kunusuru wakimbizi wajawazito kutoka Burundi

UNFPA, wadau wahaha kunusuru wakimbizi wajawazito kutoka Burundi

Hali ya afya ya uzazi katika kambi za wakimbizi wa Burundi walioko mkoani Kigoma nchini Tanzania ni mbaya limesema Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu(UNFPA) ambalo linafanya tathimini ya mahitaji ya afya katika kambi zilizoko mkoani humo. Joseph Msami na maelezo kamili

(TAARIFA YA MSAMI)

Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa hii, msaidizi wa mwakilishi mkazi wa UNFPA nchini Tanzania DK Rutasha Dadi anasema nini wanakifanya kwa sasa ili kuwasaidia wanawake ambao wana mahitaji ya kiafya mathalani wajawazito.

(SAUTI DK. RUTASHA)

Akizungumzia hali ya mlipuko wa kipindupindu Dk. Rutasha amesema juhudi zinaendelea lakini akakiri mlipuko huo umebadili mifumo ya afya.

(SAUTI DK RUTASHA)