Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yatoa wito wa kujikita kwenye kufumbua chanjo ya HIV

UNAIDS yatoa wito wa kujikita kwenye kufumbua chanjo ya HIV

Katika kuadhimisha Siku ya Uelewa kuhusu kirusi cha HIV, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Ukimwi, UNAIDS, limetoa wito wa kimataifa wa kuanza tena kujikita katika kupata chanjo dhidi ya HIV.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé amesema kuwa upatikanaji wa chanjo itakuwa hatua kubwa katika kuutokomeza ugonjwa wa Ukimwi.

Ameongeza kuwa, kumekuwa na hatua za kisayansi zinazotia moyo, na hivyo kutoa matumaini ya kupatikana chanjo dhidi ya HIV siku zijazo.

Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa chanjo dhidi ya HIV inaweza kupatikana, kufuatia jaribio la chanjo aina ya RV144 lillilofanywa mnamo mwaka 2009, na ambalo lilipunguza kiwango cha maambukizi kwa asilimia 31.