Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 150 baada ya kuanzishwa kwake, ITU bado kwenye mstari wa mbele kwa maswala ya mawasiliano

Miaka 150 baada ya kuanzishwa kwake, ITU bado kwenye mstari wa mbele kwa maswala ya mawasiliano

Leo tarehe 17 Mei ikiwa ni siku ya kimataifa ya jamii ya mawasiliano na habari, Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Mawasiliano ITU, Houlin Zhao, amesema Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Teknohama, ni msingi wa maendeleo ya siku za usoni na ni chanzo cha uvumbuzi.

Katika ujumbe wake kwa siku hiyo, bwana Zhao amesema tangu kuanzishwa kwake mwaka 1865, ITU imejitahidi kuunganisha watu na nchi duniani kote kupitia teknolojia mbali mbali, siku hizi kupitia Intanet na simu za mkononi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelipongeza shirika la ITU kwa uwezo wake wa kubaki kwenye mstari wa mbele katika maswala ya teknolojia za mawasiliano, akiongeza kwamba mapinduzi ya kidigitali yamebadilisha dunia. Hatimaye amesema teknohama zinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi na utunzaji wa mazingira.