Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu awasihi viongozi wa Asia kuokoa wahamiaji

Katibu Mkuu awasihi viongozi wa Asia kuokoa wahamiaji

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea wasiwasi wake kuhusu hatma ya wakimbizi na wahamiaji waliopwelewa kweye bahari ya Andaman na mlango wa Malakka, kati ya Myanmar, Thailand na Malaysia.

Katika taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake, Katibu Mkuu amenukuliwa akiwasihi viongozi wa ukanda wa Asia Kusini Mashariki kuwaoka wahamiaji hao na kutowakatalia kushuka.

Katika siku chache zilizopita, bwana Ban ameongea na Waziri mkuu wa Malaysia na Thailand, huku Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson akizungumza na waziri wa mambo ya nje wa Bengladesh na naibu Waziri wa maswala ya kimataifa ya Indonesia.

Katika mazungumzo yao, wamezingatia umuhimu wa kulinda maisha ya binadamu na kuheshimu sheria ya kimataifa.

Aidha wamesisitiza umuhimu wa kukubali wahamiaji hao wateremke kwenye muda mwafaka.

Hatimaye, bwana Ban na bwana Eliasson wamependekeza viongozi wote washiriki kwenye mkutano wa kikanda kuhusu swala la wahamiaji utakaofanyika hivi karibuni mjini Bangkok, nchini Thailand.