Vikundi vyenye silaha vyateka nyara raia Libya: UNSMIL

Vikundi vyenye silaha vyateka nyara raia Libya: UNSMIL

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL umesema vikundi vyenye silaha vinawajibika katika utekaji nyara raia wakiwamo watoto .

Taarifa ya UNSMIL kwa vyombo vya habari imesema kuwa utekaji nyara, mateso na uuaji ni uhalifu ikikemea vitendo hivyo ambapo pia watu wanaokabiliwa na vitendo hivyo wanaelezwa kuwa katika hatari

Ujumbe huo umesema kuwa baadhi ya raia waliotekwa nyara na vikundi hivyo vyenye silaha wamefia vizuizini ama kwa kwa kuuwawa au kuteswa hadi umauti.

Umeongeza kuwa utekaji nyara huu umeongeza mapigano na mgogoro mkubwa nakuenea kwa kundi la kigaidi la ISIL na vikundi vingine vyenya misimamo mikali.

Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umeongeza kuwa uhalifu huu umekuja siku chache baada ya mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC kuwasilisha ripoti yake kwa baraza la usalama kuhusu Libya ambayo iliangazia kudorora kwa usalama nchini humo. Ujumbe umetaka watekelezaji wa vitendo hivyo wafikishwe mbele ya mahakama hiyo.