Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umuhimu wa familia katika jamii nchini Kenya

Umuhimu wa familia katika jamii nchini Kenya

Siku ya familia duniani imekuewa ikiadhimishwa  Mei  15 kila mwaka tangu ipitishwe na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1993. Lengo ni kutoa fursa ya kuchagiza uelewa kuhusu taasisi hiyo muhimu kabisa ili kuimarisha maarifa kuhusu maswala ya kijamii, kiuchumi na mabadiliko yanayoathiri familia.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya je wanaume wanawajibika? Inalenga kuimarisha usawa wa kijinsia na haki za watoto katika familia. Aidha unapigia chepuo kuzuia ukatili katika familia kupitia sheria na mikakati na programu za kuingilia kati.

Katika ujumbe wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wa kubadili sheria na mifumo potofu ya kijadi inayowezesha wanaume kutawala wanawake na kuendeleza ubaguzi na kuzuia ufutaji wa ukatili dhidi ya kundi dhaifu zaidi katika familia. Aidha amesema wakati dunia ikiangazia maendeleo endelevu ni muhimu kwamba kila mtu asimame kwa ajili ya haki za wanawake na watoto katika familia na jamii kwa jumla. Je hali ya familia ikoje nchini Kenya?