Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya familia ikiadhimishwa, maisha ya ukumbizini yaangaziwa

Siku ya familia ikiadhimishwa, maisha ya ukumbizini yaangaziwa

Siku ya kimataifa ya familia ikiadhimishwa ijumaa hii, Umoja wa mataifa unasisistiza kuhusu umuhimu wa kuheshimu haki za wanawake na watoto ili kuwezesha ustawi wa kundi hilo ambalo limeachwa nyuma ukilinganisha nafasi ya mwanaume katika familia.Maadhimisho ya mwaka huu yenye kauli mbiu je wanaume wanawajibika? Yanataka ujumuishwaji wa wanawake katika nafasi zote ikiwamo maamuzi na pia kutoa fursa kwa watoto kwa kutowafanyia ukatili dhidi ya haki zao za msingi ikiwamo elimu na afya. John Kibego kutoka Uganda ameandaa makala kuhusu familia ya wakimbizi ndhini humo, ungana naye kujua yale wanayokabiliana nayo ukimbizini.