Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha kuanza tena mazungumzo baiana ya viongozi wa Cyprus ya Ugiriki na Uturuki:

Ban akaribisha kuanza tena mazungumzo baiana ya viongozi wa Cyprus ya Ugiriki na Uturuki:

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kuanza tena kwa mjadiliano kamili baina ya kiongozi wa Cyprus ya upande wa Ugiriki Nicos Anastasiades na kiongozi wa Cyprus ya upande wa Uturuki Mustafa Akıncı yalioanza leo Mai 15 chini ya uwezeshaji wa mshauri maalumu , Espen Barth Eide.

Huku hamasa ya kupata suluhu ikiongezeka kwa mgawanyiko wa muda mrefu wa kisiwa hicho , Katibu Mkuu amepongeza nia ya viongozi hao ya kutaka kusonga mbele bila kuchelewa katika mazingira chanya na yenye ari kama walivyojidhatiti wakati wa mlo wa usiku ulioandaliwa na mshauri maalumu Eide hapo Mai 11 mwaka huu.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa viongozi hapo kutumia fuirsa hii kufikia hatua nzuri ya kuelekea suluhu ya kudumu ambayo italeta faida kwa pande zote za Wacyprus wa asili ya Uturuki na Wacyprus wa asili ya Ugiriki.

Ban amerejelea kauli yake ya kuendelea kuwasaidia viongozi hao na juhudi zao ili kufikia muafa utakaoenda sambamba na tamko lao la Februari 11 2014 na kuzingatia maazimio ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.