WFP yakaribisha msaada wa tume ya Ulaya kwa walioathirika na machafuko Sudan Kusini:
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, leo Ijumaa limekaribisha mchango wa dola milioni 13.8 kutoka Muungano wa Ulaya ili kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa watu walioathirika na vita vinavyoendelea Sudan Kusini.Akizungumzia msaada huo mwakilishi na mkurugenzi wa WFP Sudan Kusini Joyce Luma amesema wanaushukuru Muungano wa Ulaya kwa msaada huo muhimu ambao ni dalili kwamba dunia haijawasahamu mamilioni ya watu wanaohitaji msaada Sudan Kusini.
Mchango huo wa dola Zaidi ya milioni 13 umetoka kwenye idara ya tume ya Muungano wa Ulaya ya msaada wa kibinadamu na ulinzi wa raia ECHO.
Msaada unajumuisha dola milioni 10.6 kwa ajili ya msaada wa dharura wa chakula kwa WFP kuwasaidia wakimbizi wa ndani na wengine walioathirika na mapigano kwenye majimbo ya Jonglei, Upper Nile na Unity.