Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwanja wa Lake Tanganyika wahifadhi kwa muda wakimbizi wa Burundi:UNHCR

Uwanja wa Lake Tanganyika wahifadhi kwa muda wakimbizi wa Burundi:UNHCR

Wakati jaribio la mapinduzi ya kijeshi nchini Burundi likiripotiwa kushindwa, hali ya usalama kwenye mji mkuu Bujumbura imeripotiwa kuwa ya mashaka huku ghasia zikiripotiwa hapa na pale Ijumaa ya asubuhi na ikielezwa kuwa warundi wengi zaidi wanakimbia nchi hiyo.

(Taarifa ya Assumpta)

Hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR likieleza kuwa zaidi ya watu Laki Moja wamekimbia huku idadi kubwa ikiwa imeingie Tanzania, wengine Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Msemaji wa UNHCR mjini Geneva, Karin de Gruijl amesema idadi imeongezeka zaidi siku chache zilizopita huku wengine wakiishi kwenye fukwe za ziwa Tanganyika na wengine wakisubiri kuingia nchini Tanzania ambako waliofika tayari wanapata hifadhi kwa muda kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kwa ajili ya ukaguzi wa afya na chanjo na hatimaye kwenda kambini.

(Sauti ya Karin)

 “Tunavyozungumza, malori 17 yaliyobeba vifaa muhimu kama vile vyandarua na mahema yanaelekea Kigoma kutoka bohari yetu kwenye ukanda huo na yanatarajiwa kuwasili Jumapili. Zaidi ya watu Elfu 18 wameshahamishimiwa kambini.”