Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada zaidi wa madawa na vifaa wawasili Yemen: WHO

Msaada zaidi wa madawa na vifaa wawasili Yemen: WHO

Shirika la afya duniani WHO limeongeza jitihada zake za kufikisha msaada wa dawa na vifaa vya huduma za afya nchini Yemen  wakatio huu ambapo kuna usitishaji wa muda wa mapigano.

Zaidi ya tani 20 za dawa na vifaa vya afya vimesafirishwa kwa ndege kutoka kituo cha masuala ya kibinadamu cha WHO kilichopo Dubai hadi Djibouti ambako vitapakiwa kwenye meli ya Umoja wa Matifa leo Jumatano tayari kwa safari ya kuelekea Hodeida.

Usafirishaji wa vifaa hivyo unajumuisha vifaa vya kimataifa afya ya dharura, vifaa vya waliopatwa na kiwewe, vifaa vya upasuaji,  vifaa vya ugavi, vifaa vya dharura vya  ugonjwa wa kuhara, na vifaa vya kusafisha  maji, usafi wa mazingira na vya usafi ambavyo vitawafaidi zaidi ya walengwa 120 000 .

Pia WHO inasafirisha dawa za kuzuia malaria kutoka kwenye mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi kifua kikuu na malaria zitakazotosheleza dozi 44,950 za kutibu malaria.