IOM inasaidia familia zinazokimbia machafuko Idleb Kaskazini Mashariki mwa Syria:

15 Mei 2015

Machafuko kwenye jimbo la Kaskazini Mashariki mwa Syria la Idlen lililopo mpakani na Uturuki yanaendelea .

Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA kuanzia mwishoni mwa mwezi April inakadiriwa kuwa watu 133,831 wametawanywa na machafuko hayo.

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM linagawa msaada usio chakula kutoka Damascus na Gaziantep nchini Uturuki ili kuwasaidia wakimbizi wa ndani waliotawanywa na mchafuko.

Tangu Aprili 2 IOM imewafikia wakimbizi wa ndani 27,000 na kuwagawia vifaa 7950 visivyo chakula ambavyo ni pamoja na nguo, mablanketi, vifaa vya usafi, nepi za watoto na vyandarua vya kuzuia mbu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter