Skip to main content

Mkurugenzi mkuu wa UNIDO azuru Japan kuimarisha ushirikiano na taifa hilo:

Mkurugenzi mkuu wa UNIDO azuru Japan kuimarisha ushirikiano na taifa hilo:

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO  Li  Yong, amekuwa ziarani nchini Japan, ambako amekutana na waziri wa mambo ya nje Yasuhide Nakayama, na makamu waziri wa uchumi, viwanda na biashara Yoshihiro Seki,.

Bwana Li amesema ziara yake nchini Japan ambayo imekuja katika wakati muafaka ni muhimu sana na ni ya kutanabaisha vipengee kadhaa ambavyo ni vya muhimu kwa ushirikiano baina ya UNIDO na serikali ya Japan na kuisikiliza serikali hiyo kwa mtazamo wa kubaini maeneo ambayo ushirikiano kati ya UNIDO na nchi hiyo unaweza kuimarishwa zaidi.

Ameishukuru serikali ya Japan kwa kuendelea kuisaidia UNIDO hasa kwa kutoa mchango wake kwa bajeti ya shirika hilo kwa wakati , lakini pia kwa kufadhili miradi mbalimbali ya UNIDO kwa hiyari.