Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yatiwa hofu na hali ya Burundi

Ofisi ya haki za binadamu yatiwa hofu na hali ya Burundi

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imesema inatiwa hofu na hali inayoendelea nchini Burundi katika siku bili zilizopita na inatoa wito kwa majeshi na wadau wengine kujizuia na hatua ambazo zitahatarisha maisha ya raia na kuhakikishwa wanalindwa na athari za vita.

Ofisi hiyo imesema ni dhahiri kwamba hali ya kutokuwepo utulivu huenda ikaendelea au hata kuwa mbaya zaidi endapo ghasia hazitozuiliwa wakati huu ambapo mashambulizi yameripotiwa dhidi ya vyombo vya habari vya serikali na binafsi huku vituo vya Radio na televisheni vikiharibiwa.

Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu mjini Geneva.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

“Tunatoa wito kwa kufunguliwa kwa vyombo vyote vya habari na kuheshimiwa kwa uhuru wa waandishi wa habri. Pia kuna umuhimu wa haraka wa kuhakikisha usalama wa watetezi wa haki za binadamu na wanahabari. Mfano mmoja tu ni mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu Burundi Pierre-Claver Mbonimpa, amekimbilia mafichoni baada ya kupokea vitisho vya kuuawa.”