Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yalaani mauaji ya raia 17

UNAMA yalaani mauaji ya raia 17

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan(UNAMA), umelaani vikali shmbulio mauaji ya watu 17 yaliyotokana na mashambulio mawili hapo jana ambapo wanamgambo wa Taliban wamedai kuhusika.

Katika tukio la kwanza raia 14waliokuwa wamekusanyika katika eneo la mapumziko karibu na hoteli iitwayo Palace mjini Kabul waliuwawa huku wengine kadhaa wakijeruhiwa. Raia wengine watatu waliuwawa na wawili  kujeruhiwa katika shambulio jingine katika  idara ya Haj na masuala ya dini huko Lashkargah jimboni Helmand.

Taarifa ya UNAMA imemkariri Mkurugenzi wa haki za binadamu Bwana Georgette Gagnon akisema kuwa mashambulio hayo yanayolenga raia ni ukatili wa kupindukia na kuongeza kuwa tamko la Wataliban kuhusu kuepuka kuua raia halijatekelezeka mashambulio kama hayo yanaposhuhudiwa.

Ametaka Wataliban  kusimamia ahadi zao na kuacha hima mashambulizi ya kuwalenga raia wasio na hatia.