Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukuaji uchumi jumuishi ni muhimu kwa nchi za Asia-Pasifiki-ESCAP

Ukuaji uchumi jumuishi ni muhimu kwa nchi za Asia-Pasifiki-ESCAP

Uchumi wa nchi zinazoendelea zilizoko ukanda wa Asia-Pasifiki unaendelea kuimarika ikilinganishwa na maeneo mengine duniani lakini udhaifu wa kimuundo kama vile barabara, kudumaa kwa baishara ya kimataifa vinakwamisha ustawi zaidi.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya tume ya uchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa kwa ukanda wa Asia-Pasifiki-ESCAP iliyotolewa leo ikieleza kuwa uchumi jumuishi ni msingi wa kuhakikisha ustawi endelevu kwa watu wote.

Mathalani ukuaji uchumi unatarajiwa kuongezeka kidogo tu hadi asilimia Tano nukta Tisa mwaka huu ikilinganishwa na asilimai Tano nukta Nane mwaka jana ambapo Alfred Calcagno, Afisa kutoka kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD anataja sababu.

(Sauti ya Alfred)

Uwekezaji zaidi unahitajika katika usafiri, umeme na  miuondo mbinu mingine katika nchi ambako miji inaendelea kukua. Utegemezi wa bidhaa katika nchi hizi hususan ambazo zinazalisha gesi au madini, unaathiri biashara ya kimataifa na hili ni eneo ambalo linadhoofishwa huku kusuasua kwa  mitaji  na fedha  kukifanya eneo hilo liwe katika hatari ya kuathiriwa na kushuka na kupanda kwa bei ambako hatimaye kutaathiri uchumi."