Skip to main content

Shelisheli na tiba asili dhidi ya muwasho na kuhara: FAO

Shelisheli na tiba asili dhidi ya muwasho na kuhara: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limetangaza shelisheli kama zao la asili kwa mwezi huu wa Mei likitajwa kuwa na manufaa siyo tu kiafya bali pia kiuchumi.

FAO inasema Shelisheli ambalo zao kuu maeneo ya Pasifiki lina kiwango kikubwa cha wanga na huweza kuliwa bichi au likipikwa huku, kwa mujibu wa mapishi yaliyochapishwa katika tovuti ya shirika hilo.

Kiwango kikubwa cha wanga kwenye Shelisheli kinafanya liweze kutumika badala ya unga  ngano na kutengeneza chapati. Halikadhalika utomvu wake ni tiba ya asili dhidi ya kuhara na magonjwa ya ngozi.

Mti wa mshelisheli hufaa kwa mbao za ujenzi wa nyumba na mashua na ni thabiti dhidi ya mchwa ilhali maua yake yakichomwa moshi wake hufukuza mbu.

Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo Sita ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu wa kati mita Tisa hadi 18 ambapo huanza kuzaa matunda ukiwa na miaka Sita na kuendelea kwa miaka zaidi ya 50.

Kwa sasa zao hilo ambalo asili yake kabisa ni Ocenia, limeenea hadi maeneo ya Pasifiki, tropikali ikiwemo Afrika, Amerika ya Kusini Australia, Asia na Amerika ya Kusini.