Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunafuatilia kinachoendelea Burundi, kauli ya Ban huko AU bado ni muhimu: Dujarric

Tunafuatilia kinachoendelea Burundi, kauli ya Ban huko AU bado ni muhimu: Dujarric

Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa karibu kinachoendelea nchini Burundi na tunarejelea kauli ya Katibu Mkuu Ban Ki-moon aliyotoa wakati wa mkutano wa viongozi wa Muungano wa Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia kuhusu awamu za uongozi.

Ni kauli ya msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric aliyotoa jijini New York, Marekani wakati wa mkutano na waandishi wa habari waliotaka kufahamu msimamo wa chombo hicho kuhusu hali iliyoripotiwa Burundi.

Sauti ya Dujarric)

“Unajua sidhani kama kuna mtu anafurahai au anatambua mapinduzi ya kijeshi ambayo ni uondoaji serikali madarakani kinyume cha katiba. Nadhani tuanchofahamu sasa hali inazidi kuwa ya mashaka, tunajaribu kupata taarifa ili tufahamu kinachoendelea Bujumbura. Nadhani inazidi kubainika kuwa mara kwa mara katibu mkuu amesisitiza siyo tu kwa nchi za Afrika bali pia kwingineko duniani juu ya umuhimu wa viongozi kusikiliza matakwa ya wananchi wao na kuheshimu taasisi za kidemokrasia. Bila shaka hali Burundi inabadilika hivyo tuendelea kufuatilia kwa karibu sana.”

Kwa mujibu wa Dujarric, mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kaw maziwa makuu, Said Djinnit yuko Tanzania ambako kumefanyika mashauriano kuhusu Burundi.