Skip to main content

Waasi wa ADF wamekiuka haki za binadamu DRC: Ripoti

Waasi wa ADF wamekiuka haki za binadamu DRC: Ripoti

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imebaini ukiukaji mkubwa wa haki ya kimataifa za kibinadamu kwenye maeneo ya Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Taarifa zaidi na Flora Nducha.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Kwa mujibu wa ripoti hii, vitendo hivyo ambavyo vimetekelezwa na waasi wa ADF kutoka Uganda, vinaweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Takwimu zinaonyesha kwamba raia 237 wameuawa, wakiwemo watoto 35, kati ya Oktoba 1 na Disemba 31, mwaka 2014, wakati wa mashambulizi dhidi ya vijiji 35.

Uchunguzi huo umefanyika na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu nchini DRC kwa kupitia ushaidi wa watu zaidi ya 180.

Ripoti inasema jeshi la kitaifa la FARDC linashukiwa kutekeleza pia ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa kupambana na ADF. Tayari watu 300 wamekamatwa, wakimwemo wanajeshi 33.

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Martin Kobler, amezisihi mamlka za serikali kuchukua hatua zote ili kusitisha mauaji haya ya raia.