Skip to main content

WHO yatoa ripoti ya malengo ya afya katika nchi 194:

WHO yatoa ripoti ya malengo ya afya katika nchi 194:

Mwaka huu wa 2015 ni ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia yaliyoafikiwa na viongozi wa  serikali hapo 2000 yakiwa ni muongozo wa juhudi za kutokomeza umasikini.

Takwimu za afya duniani zilizotolewa leo na shirika la afya WHO zinatathimini hatua zilizopigwa katika malengo ya milenia ya afya kwa nchi 194 , na matokeo ya tathimini hiyo ni mchanganyiko.

Kwa mujibu wa ripoti ya WHO ifikapo mwisho wa mwaka huu dunia itakuwa imetimiza malengo ya kukabiliana na maradhi kama ukimwi, malaria na kifua kikuu na kuongeza upatikanaji wa maji salama ya kunywa.

Na pia kutakuwa kumepigwa hatua kubwa katika kupunguza utapia mlo kwa watoto, vifo vya kina mama na watoto wachanga na kuboresha hali ya usafi. Dr. Ties Boermat ni mkurugenzi idara y takwimu za afya wa WHO.

 (SAUTI YA DR TIES BOERMAT)

“Bila shaka takwimu hizi zinazingatia malengo ya maendeleo ya milenia, hizi si takwimu za mwisho mwisho sababu mwaka bado haujaisha, lakini ni makadirio mazuri na thabiti na yanatupa taswira ya hali halisi ilivyo duniani katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia, kumekuwa na maendeleo mazuri na yenye kutia moyo katika kipindi cha miaka 25 , hasa katika mapambano dhidi ya ukimwi, kifua kikuu na Malaria, lakini bado tuko mbali kabisa katika kutimiza  malengo  ya MDG's”