Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano ya kikabila Darfur hayana tija: UNAMID

Mapigano ya kikabila Darfur hayana tija: UNAMID

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika jimboni Darfur nchini Sudan UNAMID umelaani vikali kukua kwa mapigano ya kikabila baina ya Ma’alia na Reziegat uliosababisha vifo vya makumi ya watu na majeruhi kutaka pande zote.

UNAMID katika taarifa yake inasema juhudi za kusaka suluhu zinaendelea ili kunusuru maisha ya raia wasio na hatia huku ujumbe huo ukisema uko tayari kusaidia serikali ya Sudan katika kuwanusuru raia zaidi ya 50waliojeruhiwa kwa kuwafiikisha Khartoum kwa matibabu.

Katika mahojiaano na idhaa hii kutoka Sudan Kaimu mratibu mkazi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA nchini Sudan, Geert Cappalaere ametaka serikali kutoa ushirikiano kwa jumuiya ya watoa misaada ya kibinadamu ili kuwafikia wahitaji na akalalama

(SAUTI GEERT)

"Nchini Sudan jumuiya ya watoa misaada ya kibinadamu  inakabiliwa na mahitaji ya zaidi ya watu milioni tano wengi wao wakiwa jimboni Darfur, kwahiyo mapigano haya mapya yanaongeza mateso ambayo watu wa Sudan wamekumbana nayo kwa zaidi ya muongo mmoja."