Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

BAN apongeza makubaliano ya amani CAR

BAN apongeza makubaliano ya amani CAR

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kwa kupitisha mapendekezo ya makubaliano  ya amani na maridhiano ya  kitaifa nchini humo pamoja na ujenzi mpya wa taifa hilo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Katibu Mkuu, Stephan Dujjaric amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuhitimishwa kwa mkutano wa kitaifa wa Bangui.

Bwana Dujjaric amefafanua kile kilichoko katika mapendekezo yaliyofikiwa

(SAUTI DUJJARIC)

"Mapendekezo yanaakisi matakwa ya watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kuweka nyuma machafuko daima na kujenga nchi ya amani na demokrasia."

Hata hivyo amesema kilichotokea wakati wa mkutano huo wa kusaka maridhiano na ujenzi mpya wa Jamhuri ya Afrika ya Kati,CAR sio maandamano bali ni makundi ya watu waliotaka kufikisha ujumbe wao na kongeza kuwa purukushani hiyo haikuzua mkutano.