Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wafuatilia ripoti za mauaji huko Huambo, Angola

UM wafuatilia ripoti za mauaji huko Huambo, Angola

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inafuatilia kwa karibu taarifa za kina kuhusu mauaji yaliyoripotiwa kwenye jimbo la kati la Huambo nchini Angola wakati huu ambapo kuna utata kuhusu idadi ya vifo na tukio lenyewe.

Msemaji wa ofisi hiyo Rupert Colville amesema kwa mujibu wa serikali ya Angola, askari polisi tisa na raia 13 waliuawa wakati wa makabiliano huko Serra Sumé wakati polisi walipojaribu kumtia nguvuni kiongozi wa madhehebu ya dini yaitwayo Luz du Mundo au mwanga wa dunia.

Hata hivyo ripoti nyingine zinadai kuwa mamia ya wafuasi wa kiongozi huyo wameuawa ikidaiwa pengine ni zaidi ya Elfu Moja na kwamba..

(Sauti ya Colville).

“Tahariri za hivi karibuni za magazeti na habari kwenye vyombo vya habari vya serikali zikishutumu madhehebu hayo zimekuwa kali na zinatia wasiwasi. Tunafahamu baadhi ya wafuasi wa madhehebu hayo na familia zao wamejificha kwa hofu ya ghasia. Tunafahamu serikali imeanza uchunguzi wa tukio hilo. Tunaisihi ihakikishe unakuwa wa maana, huru na wa kina kwa misingi ya kuhakikisha uwajibikaji.”