Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya UM ya haki za mtoto kukutana Geneva kuanzia Mai 18 hadi Juni 5

Kamati ya UM ya haki za mtoto kukutana Geneva kuanzia Mai 18 hadi Juni 5

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya haki za mtoto itakutana mjini Geneva kuanzia Mai 18 hadi Juni 5 kupitia haki za mtoto katika mataifa ya Eritrea, Mexico, Ghana, Honduras, Ethiopia, Uholanzi, Lao na Israel.

Kamati hiyo iliyo na wataalamu huru 18 inafuatilia jinsi nchi zilizoridhia mkataba wa haki za mtoto zinavyotekeleza wajibu wao wa kulinda haki za mtoto.

Kamati pia inatathimini jinsi gani mataifa yanatekeleza itifaki ya miakataba miwili ya hiyari ambayo ni ule wa kuunza watoto, ukahaba kwa watoto na ngono kwa watoto, na ule wa pili ambao ni wa kuwahusisha watoto katika vita vya silaha.

Wakati wa mkutano huo mjini Geneva wajumbe wa kamati hufanya kipindi cha maswali na majibu na jumbe za mataifa yanaofanyiwa tathimini.