Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kupeleka vyakula kwa watu 750,000 Yemen

WFP kupeleka vyakula kwa watu 750,000 Yemen

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za Binadamu imekaribisha leo uamuzi wa pande za mzozo wa kusitisha mapigano kwa muda wa siku tano nchini Yemen. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia.

(Taarifa ya Grace)

Sitisho la mapigano limeanza leo kwa muda wa siku tano, wakati idadi ya vifo nchini Yemen imezidi 800 tangu mwanzo wa mapigano.

Ofisi ya haki za binadamu imekaribisha uamuzi huo, ikisema utawezesha mashirika ya kibinadamu kufikisha misaada.

Tayari Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema litaweza kutoa mgao wa dharura wa chakula kwa watu 750,000 katika maeneo yaliyoathirika na vita, baada ya kukwama kwa sababu ya ukosefu wa mafuta.

Elizabeth Byrs, msemaji wa WFP amesema meli moja ya WFP limefika Hudayda ikiwa na lita 250,000 na mafuta na vifaa ya misaada.

“ Wakati wa sitisho la mapigano, WFP litaweka tayari vyakula maalum kwa ajili ya watoto 25,000 wenye umri chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito, Uwiano wa utapiamlo wa watoto nchini Yemen ni mkubwa kuliko zote duniani. Nusu ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano wamedumaa."

Wakati huo huo Mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed, amewasili nchini humo leo,