Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO kuzindua ripoti ya hali ya ajira duniani mwaka 2015 hapo Mai 19

ILO kuzindua ripoti ya hali ya ajira duniani mwaka 2015 hapo Mai 19

Shirika la kazi duniani ILO limepanga kuzindua ripoti yake ya mwaka kuhusu hali ya ajira na jamii mwaka 2015 wiki ijayo hapo Jumanne ya Mai 19.

Ripoti ya mwaka huu inajikita katika njia ambazo mabadiliko ya mifumo ya kazi na mashirika ya kazi yana kuwa na athari kwa makampuni ya biashara, wafanyakazi na ulimwengu mpana wa masuala ya kazi.

Ripoti itatoa takwimu mpya kuhusu malipo na mishahara ya ajira,kikanda na kimataifa na kuweka bayana kuhusu mikataba ya muda mfupi na ya vipindi maalumu.  Ripoti hiyo pia inaangalia migawanyiko ya ugavi wa kimataifa na kutoa takwimu juu ya idadi ya wafanyakazi wanaohusika.

Na hatimaye itajumuisha mapendekezo ya sera za jinsi gani ya kupunguza ongezeko la kutokuwepo usawa kupitia mifumo ya kijamii na sharia za ajira.