Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya mwandishi wa Mexico Armando Saldaña Morales:

Mkurugenzi mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya mwandishi wa Mexico Armando Saldaña Morales:

Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu sayansi na utamaduni UNESCO Bi Irina Bokova leo Jumanne ametaka ufanyike uchunguzi dhidi ya mauji ya mwandishi habari Armando Saldaña Morales nchini Mexico, akisistiza haja ya kukomesha ukwepaji sharia kwa uhalifu dhidi ya wafanyakazi wa vyombo vya habari.

Amesema analaani vikali mauaji ya Armando Saldaña Morales na kuitaka serikali ya Mexico kuchukua hatua zinazostahiliand , kwani uhalifui dhidi ya waandishi wa habari unathiri jamii nzima na kuziia uwezo wa raia kuwa na chaguo la kupashwa habari na hivyo ni muhimu kuchukuliwa hatua uhalifu huo.

Mai nne polisi walikuta mwili wa Saldaña Morales kwenye jimbo la Oaxaca. Saldaña Morales alikuwa mtangazaji wa kipindi cha habari kwenye Radio ijulikanayo kama La Ke Buena 100.9 FM kwenye mji wa Tierra Blanca katika jimbo la Veracruz .

Pia alifanya kazi kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo kwenye El Mundo de Córdoba, El Sol de Córdoba, La Crónica de Tierra Blanca na Radio Max.