Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mengi yahitajika kulinda misitu Afrika:Kowero

Mengi yahitajika kulinda misitu Afrika:Kowero

Bado tunazidi kupoteza misitu bara la Afrika ikilinganishwa na bara nyingine kwa mfano Ulaya ambako ukataji miti unakwenda sambamba na upanzi, hiyo ni kauli ya Godwin Kowero mkurugenzi wa Shirika la Misitu African Forest Forum liloko Nairobi Kenya kandoni mwa kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu misitu, ambalo limeingia wiki ya pili hapa mjini New York.

Ametaja Swaziland kama mfano wa nchi ambazo zimeshuhudia ongezeko la misitu barani Afrika huku akisema kwamba kichochezi cha upungufu huu ni

(Sauti ya Kowero)

Kwa mantiki hiyo amesema kwamba ni muhimu viongozi na watendaji wakuu serikalini wakabadilisha mtazamo wao ili kulinda misitu na kutambua umuhimu wake.