Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wahitaji trilioni za dola kutekeleza ajenda ya maendeleo

Umoja wa Mataifa wahitaji trilioni za dola kutekeleza ajenda ya maendeleo

Ajenda ya Maendeleo endelevu itakayoamuliwa mwaka huu kwa kipindi cha miaka 15 ijayo haitahitaji bilioni za dola, lakini trilioni, amesema Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maswala ya Kiuchumi na Kijamii, Wu Hong-Bo.

Akihojiwa na  idhaa hii, amesisitiza umuhimu wa kufadhili ajenda ya maendeleo.

“ Malengo 169 ya maendeleo yanaangazia kila sehemu ya maendeleo yetu. Kwa hiyo yakitekelezwa, kila mtu kwenye dunia hii, atafaidika. Na mpango mzuri huhitaji pesa ya kuutekeleza. Kutokana na hiyo, tunapenda kuona kwamba tunahitaji fedha zaidi kuliko tulizonazo. “ 

Bwana Wu Hong-Bo amesema ufadhili wa maendeleo unapaswa kubadilika sasa kutokana na upungufu wa pesa duniani, mahitaji yakizidi kuongezeka na hali ya kiuchumi ikipata nafuu pole pole.

Ameeleza kwamba kongamano la kimataifa kuhusu ufadhili wa maendeleo litakalofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia mwezi Julai litaangazia jinsi ya kushirikisha kila aina ya chanzo cha ufadhili, ikiwemo serikali za mitaa, kipato cha ushuru cha kitaifa, ushirikiano na sekta binafsi…