Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia itakuwa na nafasi nzuri ya kukabiliana na ebola endapo itazuka tena:Chan

Dunia itakuwa na nafasi nzuri ya kukabiliana na ebola endapo itazuka tena:Chan

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO Bi. Margaret Chan amesema endapo ugonjwa wa ebola utazuka tena basi wakati huo dunia itakuwa na nafasi nzuri ya kuweza kukabiliana nao. Taarifa Zaidi na Grace Kaneiya

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Akihutubia katika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu utafiti na maendeleo ya ebola Bi chan amesema juhudi za utafiti na maendeleo ya ebola  yamefanikiwa kukusanya watu, taasisi na rasilimali katika njia ambayo haijawahi kuonekana hapo kabla.

Ameongeza kuwa matekeo yamekuwa ni mazuri katika vinginevyo janga la kibinadamu. Nyenzo mpya zimeundwa katika muda mfupi ingawa fursa ya kuzifanyia majaribio baadhi ya nyenzo hizo inatoweka.

Jumamosi WHO imetangaza kuwa Ebola imemalizika nchini Liberia jambo ambalo ni mafanikio makubwa kabisa tangu kuzuka kwa ebola mwaka 1976.

Kabla ya mlipuko huu wa karuibuni Ebola ilikuwa inachukuliwa kama maradhi ya nadra na hayakueleweka vyema.

Bi Chan amesema hatua iliyofikiwa sasa kuapambana na ebola ni mchango mkubwa wa kisayansi na pia maandalizi ambayo ymetoa funzo kubwa endapo utazuka tena.