Skip to main content

Zaidi ya watu 300,000 hawana msaada wa kuokoa maisha jimbo la Unity Sudan Kusini:Lanzer

Zaidi ya watu 300,000 hawana msaada wa kuokoa maisha jimbo la Unity Sudan Kusini:Lanzer

Naibu mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini Tobby Lanzer amesema watu Zaidi ya 300,000 wameachwa bila msaada wowote wa kuokoa maisha kwenye jimbo la Unity nchini humo. Priscilla Lecomte na taarifa Zaidi

(Taarifa ya Priscilla)

Kwa mujibu wa Bwana Lanzer machafuko yanayoendelea jimboni Unity yamesababisha mashairika yote yasiyo ya kiserikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa kuondoa wafanyakazi wake hasa kutoka eneo la Leer na mengineyo huku operesheni za kibinadamu kwenye eneo la Bentiu kusini mwa jimbo la Unity zikisitishwa kabisa.

Hali hiyo imesababisha raia Zaidi ya 300,000 ambao wanahitaji misaada ya haraka ikiwemo chakula na huduma za afya kukosa msaada huo muhimu wa kuokoa maisha.

Kuzuka upya kwa machafuko jimboni humo kumekuja wakati ambapo akiba ya chakula inapungua na ni wakati ambapo watu wanatarajiwa kuanza kupanda amzao. Mashirika ya misaada yamesema yatarejea kwenye jimbo hilo kuendelea na shughuli zake mara tuu hali itakapotengamaa na kuwa salama kufanya hivyo.