Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shehena zaidi za mafuta kuwasili Yemen:WFP

Shehena zaidi za mafuta kuwasili Yemen:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema shehena zaidi za mafuta na vyakula vya misaada zinatarajiwa kuwasili nchini Yemen katika siku chache zijazo ili kuondoa mkwamo uliosababisha baadhi ya wananchi kukosa mahitaji yao muhimu wakati huu ambapo mashambulizi yamewatumbukiza katika njaa na shida.Mwakilishi  wa WFP nchini humo Purnima Kashyap amesema hayo wakati akipokea shehena ya mafuta iliyowasilishwa kwa meli kwenye mji mkuu Sana’a.

Amesema shehena hiyo ya lita Laki Tatu itawezesha WFP kuendeleza operesheni zake zilizokwama kutokana na uhaba wa mafuta.

WFP huhitaji lita Milioni Moja za mafuta kila mwezi ili kusambaza misaada kwa wahitaji ambapo katika wiki tatu zilizopita imeweza kufikisha misaada kwa zaidi ya watu Milioni Moja huku watu Milioni 12 hawafahamu mustakhbali wao.